Mane, Mahrez, Salah kuwania tuzo la mchezaji bora bara Afrika

CAF
CAF
Shirikisho la Soka la Afrika limetangaza wanaume watatu ambao wameteuliwa kuwania tuzo la mchezaji bora wa mwaka 2019 ambao ni nyota wa Algeria, Riyad Mahrez, Sadio Mane wa Senegal na Mohamed Salah wa Misri.

Mane na Salah wameisaidia Liverpool kushinda kombe la dunia la Fifa huku ikitarajiwa kuwa huenda Salah akashinda tuzo hilo kwa mara ya tatu mtawalia.

Chelsea itazishinda Manchester United na Liverpool katika kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 19, kwa sababu wako tayari kufikia dau la uro milioni 120 iliyotolewa na Borussia Dortmund.

Mikel Arteta alikubali kuwa kocha mkuu wa Arsenal baada ya kukosa kupata hakikisho kutoka kwa Manchester City kwamba atakuwa mrithi wa Pep Guardiola katika uwanja wa Etihad.

Lazio iliicharaza Juventus 3-1 hapo jana na kushinda kombe la Italia kwa mara ya tano huku kukiwa na historia ya maandamano ya kisiasa kwenye mchezo huo uliofanyika nchini Saudi Arabia.

Senad Lulic alifungia Lazio bao katika dakika ya 73 baada ya Paulo Dybala wa Juve kuziba bao la Luis Alberto katika uwanja wa Riyadh King Saud.

Kiungo wa kati wa Juventus Rodrigo Bentancur alifukuzwa kutoka uwanjani kwa kosa la pili, na kupelekea mkwaju wa free kick. Hii ilikuwa ni mara ya pili katika miaka mitatu Lazio wamewalaza Juventus katika michuano ya Super Cup.

Kiungo wa kati wa Tottenham wa miaka 27,raia wa Denmark, Christian Eriksen yuko tayari kukataa uhamisho wa kwenda Manchester United mwezi Januari, licha ya kutokuwa na mkataba wowote msimu ujao.