Tottenham, Arsenal na Man United wapigania sajili ya beki Samuel Umtiti

umtiti
umtiti
Tottenham, Arsenal na Manchester United wanapigana vikumbo kutaka kumsajili beki wa kati Samuel Umtiti, 26, na klabu ya Barcelona inaonekana imedhamiria kumsajili Mfaransa huyo. (El Desmarque - in Spanish)

Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito - via Metro)

Chelsea sasa wanamlenga mlinzi wa West Ham Issa Diop na wanatazamiwa kutuma dau la usajili la pauni milioni 40 kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 22. (Express)

Manchester United wanaaminika kutaka kumsajili beki wa klabu ya Hellas Verona ya Italia na raia wa Albania Marash Kumbulla, 19. (Star)

Ajax wanapanga kumrudisha beki Matthijs de Ligt, 20, kwa mkopo licha ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kumuuza Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. (A Bola - in Portuguese)

Chelsea inaonekana haipo tayari kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, huku meneja Frank Lampard akiona mchezaji huyo haendani na kikosi chake. (90min)

Crystal Palace wamekataa kumuuza Zaha kwa vigogo wa Ujerumani Bayern Munich. (Guardian)

Tottenham wamejiunga kwenye mbio za kutaka kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24, huku Milan wakitaka dau la pauni milioni 30. (Guardian)

-BBC