Malkia stirkers walishinda kwa seti za 25 -15 , 25- 21 na 25-12, na kumaliza mbele ya wenyeji Cameroon ambao walimaliza wa pili. Kenya imefuzu kwa michezo ya Japan mwaka 2020 na wanarejea chini ya kocha mkuu Paul Bitok baada ya miaka 15.
Ndoto ya waogeleaji wa Kenya kushiriki katika michezo ya Olimpiki huenda isitimie baada ya shirikisho la uogeleaji nchini FINA kuipiga marufuku shiriskiho la uogeleaji la Kenya.
Marufuku hiyo inatokana na ukosefu wa ofisi iliyo imara, baada ya kukosa kufanya uchaguzi tangu mwaka wa 2014. Kulingana na sheria za Fina, wanachama wote wanahitajika kufanya uchaguzi angalau baada ya miaka miwili jambo ambalo Kenya haijatimiza.
Agenti wa Gareth Bale anasema mchezaji huyo hataondoka Real Madrid katika kipindi cha uhamisho wa Januari wala mwishoni mwa msimu. Kocha wa Madrid Zinedine Zidane alijaribu kumuuza Bale mwanzoni mwa msimu huku akidai hayuko katika mipango yake, lakini alibadili nia na kumweka katika timu ya kwanza. Bale ana mkataba hadi msimu wa mwaka 2022 na ni vilabu chache ambavyo vinaweza kumlipa kwani anapata pauni laki 6 kama marupurupu.
Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Kenya Peter “Pinchez” Opiyo amejiunga na timu ya daraja la pili Nairobi City Stars. Pinchez ambaye anaondoka kutoka klabu ya Finland SJK hapo awali alichezea Gor Mahia, Tusker na Afc Leopards, ameandikisha mkataba wa miezi 18 na vijana hao wa Kawangware. Afisa mkuu mtendaji wa Stars Patrick Korir anadai Pinchez ataongeza udhabiti katika kikosi hicho.
Manchester United imekubali kuwa haitafanikiwa kumleta Old Trafford kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27. Wakati huo huo Tottenham Wameafikia mkataba wa pauni milioni 28 kumnunua mshambulizi wa AC Milan na Poland Krzysztof Piontek mwenye umri wa miaka 24
Kocha wa Gor Mahia Steven Polack alituzwa kwa kuwa kocha bora wa ligi ya KPL mwezi Novemba, na kunyakua taji hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kunyakua lile la mwezi Oktoba. Mzaliwa huyo wa Uingereza alishinda mechi tatu mtawalia na kujizolea alama tisa, zaidi ya makocha wenzake Robert Matano wa Tusker, Zedekaih Otieno wa KCB . Alitunukiwa shilingi elfu 75.
Kwingineko Kiungo wa Manchester United Ashley Young amekataa mkataba mpya wa mwaka mmoja, huku akiaminiwa kutaka kuondoka Old Trafford katika dirisha dogo la uhamisho la mwezi huu.
Mzaliwa huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 34 amesalia na miezi sita katika kandarasi yake na amekua akihusishwa na klabu ya Italia Inter Milan. Hata hivyo kocha mkuu Ole Gunnar Solskjaer anataka asalie United kwani ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa ambaye anaweza kucheza kama mlinzi.