Suarez hatacheza kwa kipindi cha miezi 4 baada ya kufanyiwa upasuaji

upasuaji
upasuaji
Mshambulizi wa Barcelona Luis Suarez hatacheza kwa kipindi cha miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti. Suarez alifanyiowa upasuaji kwenye goti lilo hilo mwishoni mwa msimu uliopita, amechezea Barcelona mechi 23 msimu huu na kufunga mabao 14.

Alicheza mechi nzima, Barca waliponyukwa mabao 3-2 na Atletico Madrid katika nusu fainali ya kombe la Uhispania siku ya ijumaa.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ameonyesha nia ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22. Kwingineko mshambuliaji wa Kiingereza wa Crystal Palace, Connor Wickham mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kujiunga na Sheffield Jumatano kwa mkopo kufuatia kuwasili kwa Cenk Tosun wa miaka 28, katika uwanja wa Selhurst Park.

Manchester City  jana iliendeleza ubabe wao walipowanyuka Aston Villa mabao 6-1 katika ligi ya Uingereza. Sergio Aguero mabao matatu na kuwa mfungaji mabao bora zaidi ugenini, kwa kumpiku gwiji wa Arsenal Thiery Henry ambaye ana mabao 175 katika ligi ya Primia.

Ni wachezaji watatu tu Alan Shearer, Wayne Rooney na Andy Cole ambao wako juu yake katika orodha ya ligi ya Primia. Matokeo hayo yanaiweka City katika nafasi ya pili, nafasi ya juu zaidi wamekuwepo baada ya mechi tangi mwezi Novemba.

Kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, ambaye mkataba wake unafikia mwisho, amekubali kuichezea Inter Milan kwa mkataba wa miaka minne na nusu huku Spurs ikitaka kumuuza mchezaji huyo, wa umri wa miaka 27 kwa kitita cha pauni milioni 17 mwezi Januari.

Kwingineko Barcelona imefanya mawasiliano na Mauricio Pochettino kuhusu kuchukua nafasi ya Ernesto Valverde kama kocha. Raia huyo wa Argentina hayuko kazini baada ya kutimuliwa na Tottenham mwezi Novemba.

Tusker jana iliongeza uongozi kileleni mwa jedwali la KPL kwa kuwanyuka Bandari mabao 2-1 mjini Mombasa. Bandari waliongoza kunako kipindi cha kwanza kupitia kwa Wycliffe Ochomo kabla ya wanamvinyo kusawazisha kupitia kwa Hashim Sempala baada ya mapumziko. Brian alifungia Tusker bao la ushindi na kuwapa alama zote tatu.

Kwingineko Gor Mahia walinyukwa 2-1 na Kakamega Homeboyz uwanjani Bukhungu. AFC Leopards waliwafunga Wazito mabao 2-0 huku Ulinzi Stars wakiwanyuka Western Stima 3-2.