Pongezi "gwiji"Paul Were kuhamia Ugiriki

Mchezaji Paul Were ambaye anafahamika sana  kwa  uchezaji wake  hodari  wa mpira wa kandanda haswa katika kilabu inayosakata dimba humu nchini AFC Leopards ametangaza kuondoka klabuni humo rasmi.

Were akiandika ujumbe wake wa kushukuru uongozi wa klabu hiyo katika mtandao wake wa jamii ameshukuru kila mmoja aliyefanikisha ukuwaji wake wa soka alipokuwa anaitumikia Ingwe.

Aliandika na kusema,

" Nataka kuchukua fursa hii kushukuru kila mmoja wa klabu cha FC Leopards kwa yale ambayo tumefanya pamoja tangu siku ya kwanza," Aliandika Paul.

Nduru za kuaminika zilitufahamisha kuwa mchezaji huyo wa FC Leopards anasafiri katika katika taifa la Ugirigi kujiunga na klabu moja inayosakata kwenye ligi kuu ya taifa hilo

Hakueweza kuwasahau mashabiki wake bali aliwashukuru na kuwaambia kuwa atawakosa kwa mno yaani kwa lugha ya kimombo(miss).

"Sitasahau pia mashabiki wangu ambao walinipa msaada mkubwa endapo nipo katika uwanja nikicheza ama nikiwa sipo kwenye uwanja,"  Aliongeza Were.

Mashabiki na wachezaji wa Ingwe nao hawakusita kuonyesha upendo wao kwa kiungo huyo mshambulizi kwani walimsihi kuendelea na bidii hiyo aliyokuwa nayo alipokuwa anaichezea Leopards.

Were hakusita bali aliandika katika mtandao huo huo na kuwaaga wenzake

"Familia yangu mpya, siwezi nikangoja kucheza mchuano wangu wa kwanza," Aliandika Paul.
trevor willis
 Welcome ! Work hard get a break and you can be great at the ding !
R. Ö. Z. Z. I. E.
Congratulations
#NajuaUnajua
Congratulations more higher you will go
Eli Shere
Congratulations, give it your all!!
iampetervic

I know this is your way into the premier league.well done Timbe.