Liverpool bado ina uwezekano mkubwa wa kutwaa taji hata baada ya ligi kuahirishwa

mabingwa
mabingwa

Liverpool bado ina uwezekano mkubwa wa kutwaa taji la ligi ya Premia hata wakati ambapo coronavirus imesababisha msimu kuahirishwa. (Telegraph)

Naibu mwenyekiti wa West Ham United Karren Brady amesema kuwa msimu wa ligi ya Premia unastahili kufutiliwa mbali kabisa ikiwa hakuna mechi zingine zitakazochezwa. (Sun)

Kocha wa Leeds United Marcelo Bielsa TEMP ameamua kwamba kikosi chake kitakuwa kinafanya mazoezi katika wakati ambapo msimu wa ligi ya Premier umeahirishwa kwa sababu ya virusi vya Corona. (Mail).

Vilabu vingi vimekumbwa na changamoto katika hatua yao ya kufuatilia kwa karibu wachezaji ambao huenda wangetaka kuwasajili kwa sababu ya marufuku ya usafiri, mechi kuchezwa katika maeneo yasiyoruhusiwa watu na kuahirishwa kwa ligi. (Independent)

Ligi ya Champions huenda ikakamilika na robo fainali huku nusu fainali ikichezwa katika ligi nyingine. (Mirror)

Vilabu vinavyoshiriki ligi ya Premia huenda vikataka kucheza msimu utakapoanza tena Aprili kwa sababu ya wasiwasi wa hali ya wachezaji wao na uadilifu wa mashindano hayo. (Mail)

West Ham na Tottenham Hotspur zinashinikizo la kumaliza michezo yao ya nyumbani huku michezo mingi ya msimu wa joto ikiwa tayari imeshapangiwa kuchezwa katika viwanja vyao. (Mirror)

Arsenal sasa inafikiria uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Wolves Diogo Jota, 23. (Mail)

Juventus imemlenga Houssem Aouar, 21, kama kiungo wa kati mbadala iwapo itamkosa mchezaji wa Manchester United Paul Pogba, 26.(Calciomercato - in Italian)

Chelsea inafuatilia kwa karibu kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, katika uhamisho wa bila malipo. (Metro)

Manchester United wako kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach, kiungo wa kati wa Switzerland Denis Zakaria, 23, ambaye pia anawindwa na Liverpool, Atletico Madrid na Borussia Dortmund.(Sky Germany, via Mirror)

-BBC