'Ni upuzi iwapo FKF itahitimisha ligi.' Matano na Kimani wasema.

matano
matano
NA NICKSON TOSI

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Tusker Robert Matano na mwenzake wa AFC Leopards Anthony Modo Kimani wamesema iwapo shirikisho la soka nchini FKF  na KPL yataamua kuhitimisha ligi basi itakuwa kinyume na matarajio ya wengi na hata kuathiri wachezaji kisaikolojia.

Waandalizi wa KPL hawajatoa tarehe mwafaka ya kurejelea kwa ligi hiyo tangu kusitishwa mwezi jana na kufikia sasa Gor mahia wanaongoza kwa alama 54 baada ya kucheza mechi 23.

Wakati uo huo, Matano amepusilia mbali madai ya kuwatunuku Gor taji kulingana na alama ambazo wako nazo iwapo ligi ya KPL itasimamishwa .

Kwa upande wake Kimani, amesema itakosesha wengi ladha na litakuwa swala la kusikitisha iwapo KPL na FKF wataafikia uamuzi huo.

Kimani anasema, katika ligi zingine kama ya Ubelgiji, hakuna vile klabu zingine zingefikia viongozi wa ligi kuu ya taifa hilo kutokana na mwanya mkubwa wa alama baina ya wapinzani.

Ligi ziyingi ulimwenguni zimesitishwa huku kukiwa na hofu kuwa huenda msimo huu wa ligi nyingi ukatupiliwa mbali na kuanza upya kutokana na virusi vya Corona.