Spoti: Chelsea wako katika mazungumzo ya kumsajili Coutinho

_111716041_acdba343-91a5-4447-a3f6-385fd1b70f1e
_111716041_acdba343-91a5-4447-a3f6-385fd1b70f1e
Chelsea wapo katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazili Philippe Coutinho.

Mkusanyiko wa habari za spoti;

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, amekanusha kwa kupitia mitandao ya kijamii ripoti kuwa ana mpango wa kuhamia klabu ya Inter Milan. (Instagram)

Klabu ya Everton inaamini kuwa mustakabali wa kucheza chini ya kocha Carlo Ancelotti unaweza kumshawishi kiungo wa Aston Villa Jack Grealish, 24, kuhamia klabu hiyo. (Football Insider)

Klabu ya AS Roma imempa nafasi kiungo wa Chelsea Pedro, 32, kujiunga na kikosi chake mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wa mchezaji huyo na Chelsea utakuwa unafikia kikomo. (Mirror)

Beki wa pembeni wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 25, anatakiwa na klabu ya Barcelona katika makubaliano ambayo Barceola pia itawapa City beki raia wa Ureno - Nelson Semedo, 26. (Telegraph, subscription required)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema anamipango "miwili ama mitatu tofauti" juu ya dirisha la usajili lijalo. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Rivaldo, 47, amemshauri mshambuliaji nyota wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu. (Betfair)

Arsenal na Manchester United wapo katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ufaransa Corentin Tolisso, 25. (Foot Mercato, in French)

Kipa wa zamani wa Nigeria Dosu Joseph anasema mshambuliaji Odion Ighalo, 30, amefanya vya kutosha ili kusajiliwa moja kwa moja na Manchester United Shanghai Shenhua.. (Goal.com)

-BBC