Maruoane Fellaini aruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata nafuu kutokana na Corona

fellaini_px
fellaini_px
NA NICKSON TOSI

Mchezaji wa kitambo wa Manchester United ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Shandong Luneng ya Uchina ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kulazwa kwa majuma 3 kutokana na janga hatari la Corona ambalo alikuwa ameambukizwa.

Fellaini wa miak  32 atajitenga na watu wengine kwa siku 14 hata baada ya kupona ili kubaini iwapo angali na virusi hivyo.

Ifahamike kuwa, ndiye mchezaji pekee katika ligi kuu ya Uchina kupatikana na virusi hivyo.

Fellaini aliruhusiwa kujiunga na klabu hiyo ya Uchina mnamo Februari kwa dau la euro milioni  7.2 na kufikia wakati ligi ya Uchina ilipokuwa inasitishwa kwa muda alikuwa amefunga magoli 12 kwa mechi 34.