Michezo, Mauricio Pochettino yupo radhi kufanya mazungumzo na Newcastle United

NA NICKSON TOSI

Mkufunzi wa zamani wa klabu ya Tottenham hotspurs Mauricio Pochettino inaripotiwa kuwa yupo tayari kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Newcastle, taarifa ambazo zimechapishwa na jarida la Daily Star.

Kumekuwepo na gumzo kuwa kampuni moja kutoka Saudi Arabia inakaribia kununua klabu hiyo ya Newcastle na kuifanya kuwa miongoni mwa vilabu tajiri zaidi katika ligi ya primia ya Uingereza.

Massimilliano Allegri ni mkufunzi mwengine anayepigiwa upato kuchukuwa mikoba ya uongozi wa klabu hiyo makubaliano ya kuiuza yatakapokuwa yameafikiwa baina ya pande zote mbili.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO