'Sijakataa wachezaji wa Derby Kukatwa mishahara.' Wayne Rooney asema

_111915179_whatsubject
_111915179_whatsubject

NA NICKSON TOSI

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Wayne Rooney ametupilia mbali wazo kwamba amewashauri wachezaji wenza katika klabu ya Derby kukataa wito wa viongozi wa klabu hiyo wa kutaka wapunguziwe mishahara yao majira haya.

Rooney wa miaka 34 amekuwa akifanya mazungumzo na uongozi wa Derby kuhusiana na hatua hiyo japo hakuna chochote kilichoafikiwa kuhusiana na mazungumzo hayo.

Agizo la Derby la kutaka wachezaji wapunguze mishahara yao ilipuuziliwe mbali na wachezaji hao baada ya uamuzi wa PFA wa kusema wachezaji wasishurutishwe kupunguza mishahara.

Matamshi eti Rooney amekataa kupunguza mshahara wake ni taarifa za kupotosha umma na zisizofaa kamwe. Amesema msemaji wa mchezaji huyo akiwa kwa mahojiano na shirika la habari la BBC.