Janga la Corona limenisaidia kupona jeraha -Shakava asema

unnamed (10)
unnamed (10)
NA NICKSON TOSI

Mlinzi wa zamani wa klabu ya humu nchini Gor Mahia, Haron Shakava amesema kutokana na janga ambalo limeathiri mataifa mengi ulimwenguni na hata kufanya ligi nyingi kusitishwa kwa muda, limemfanya kupona jeraha la mguu ambalo alikuwa nalo.

Shakava ambaye anaichezea klabu ya Zambia ya Nkana alikuwa anatarajiwa kukosa mkondo wa pili wa ligi kutokana na jeraha alililopata akiwa mazoezini na timu hiyo yake.

Shakava na wachezaji wenza wa Kenya watatu walioamua kurejea nchini baada ya mashirikisho mengi ya ligi tofauti kusitisha ligi kutokana na corona.

Miongoni mwa wachezaji wanaocheza katika ligi ya Ghana na hutoka humu nchini ni kama  Musa Mohammed, Duke Abuya na Duncan Otieno.

Shakava ameongeza kuwa kutokana na janga hilo, limemfanya kuwa karibu na familia yake.

Wakati uo huo, Shakava amewataka wachezaji wa humu kuendelea na mazoezi ya ziada ili kuwa tayari wakati ligi zote zitakoporejelewa.