PSG Watawazwa kama mabingwa wa Ufaransa

NA NICKSON TOSI

Klabu ya PSG inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Ufaransa imetawazwa kama washindi wa ligi hiyo baada ya serikali ya Ufaransa kuongeza amri ya kupiga marufuku watu kukusanyika katika hafla tofauti.

PSG walikuwa wanaongoza ligi hiyo kwa wingi wa alama 12 na walikuwa wamesalia na mechi moja ya akiba kuicheza ndio kufikia mechi sawa ambazo timu zingine zilikuwa zimecheza.

Ushindi wa taji hilo unaifanya PSG kushinda mataji 9 ya ligue 1 kufikia sasa.

Serikali ya Ufaransa iliamua kuongeza muda wa kutaka watu kujitenga na maeneo ya mikutano hadi septemba.