Marcos Rojo kujua hatima yake baada ya kukiukja agizo la serikali ya Argentina

NA NICKSON TOSI

Manchester United itafanya kikao na mlinzi Marcos Rojo kuhusiana na hatua yake ya kuvunja sheria za kutotoka nje za taifa la Argentina.

Rojo ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Estudiantes, alionekana na marafiki wenzake wakiwa kwa mkahawa mmoja wakivuta banki na kubugia mvinyo licha ya serikali ya Argentina kupiga marufuku watu kutotoka nje ili kuzuia maambukizi zaidi ya Corona.

Rojo sasa anajiunga na wachezaji wengine wa ligi kuu ya Uingereza kama Jack Grealish, Kyle Walker, Moise Kean ambao wanakumbwa na mashtaka ya kukiuka agizo la serikali ya Uingereza la kutaka wananchi wake kutotoka nje .

Sheria za watu kusalia makwao katika taifa la Argentina zitasalia hadi Mei 1o.