Daniel Ricciardo kujiunga na timu ya McLaren msimu mpya wa Formula one 2021

EX-BpCVX0AENypl
EX-BpCVX0AENypl
Daniel Ricciardo anatarajiwa kujiunga na timu ya Mclaren inayoshiriki katika michezo ya Formula One akichukua nafasi iliyoachwa na Carlos Sainz aliyejiunga na Ferrari.

Mabadiliko hayo yametangazwa na wasimamizi wa kampuni hizo kama njia ya maandalizi kwa msimu mpya wa Formula One.

Ricciardo atashirikiana na  Briton Lando Norris, huku  Sainz akitarajiwa kurithi mikoba iliyaochwa na bingwa mara nne wa mashindano hayo Sebastian Vettel aliyetangaza mapema wiki jana kuwa ataondoka kwa timu ya Ferrari msimu huu utakapomalizika.

Mkuu wa McLaren  Zak Brownamesema  Ricciardo ataleta mabadiliko makubwa katika timu hiyo japo akasema Sainz alikuwa ameafikia viwango vikubwa.

Naye mkuu wa kampuni ya Ferrari  Mattia Binotto aliongezea kuwa Sainz yuko na kila kitu kinachomfanya kujiunga na timu hiyo.

"had proved to be very talented and has sown that he has the technical ability and the right attributes". amesema Binotto

Vettel alitangaza kuwa ataondoka kwenye kikundi cha Ferrari baada ya msimu kumalizika.