Nicholas Musonye atangaza azma ya kuwania urais kiti cha FKF

EYC7hKnWkAIF52Y
EYC7hKnWkAIF52Y
Aliyekuwa katibu mkuu swa shirikisho la soka CECAFA Nicholas Musonye amesema kuwa atawania nafasi ya kuwa rais wa shirikosho la soka nchini FKF mwaka huu wakati ambapo uchaguzi wa shirikisho hilo utakapokuwa ukifanyika .

Musonye amekuwa akimezea mate nafasi hiyo tangu alipohitimisha mkataba wake wa kuhudumu kama katibu mkuu wa CECAFA.

Uchaguzi wa FKF nchini umekuwa ukikumbwa na utata hali iliyopelekea shirikisho la soka duniani FIFA kuipa Kenya makataa ya kuandaa uchaguzi huo ama ipigwe marufuku .

Tumekuwepo na shida ya uongozi nchini haswa katika sekta ya michezo baada ya Nick Mwendwa kuwatangaza Gor Mahia kama washinndi wa ligi kinyume na matarajio ya wengi.

Wenyekiti wa vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu ya KPL  walielekea mahakamani kupinga hatua hiyo wakisema hawakujumuishwa wakati uamuzi huo ulipoafikiwa na FKF.

Hatua ya FKF kuwapa Gor taji ilipingwa pia na wasimamizi wa ligi nchini KPL ambao walisema wako na wajibu wa kutangaza kama ligi hiyo itaendelea ama la.

Kupitia kwa mkurugenzi mkuu wa KPL Jack Oguda, hatua ya Mwendwa ilikuwa kinyume na sheria.

Swali ni je, Nicholas Musonye atakomboa mgogoro wa FKF ambao umekuwepo kwa muda?