Sirudi kucheza mimi! Nahodha wa Watford Troy Deeney asema

_112289161_deeney
_112289161_deeney
Kutokana na hatua ya ligi kuu ya Uingereza kuiga mifano ya ligi nyingine za ughaibuni ambazo zimeanza kurejelea hali yake ya kawaida, baadhi ya wachezaji wamekashifu hatua hiyo wakisema huenda itaweka famila zao hatarini  kwa kuambukizwa virusi hatari vya coroni.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamesema hawatarejea kucheza kutokana na hali ilivyo ni nahodha wa klabu ya Watford inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Uingereza Troy Deeney. Deeney amewaambia wakuu wa klabu hiyo kuwa mwanawe wa miezi mitano mvulana amekuwa na matatizo ya kupumua na hivyo kuenda kucheza wakati ambapo virusi hivyo vimeathiri Uingereza itatia maisha ya mwanawe hatarini.

"I'm not even talking about football at the moment - I'm talking about my family's health," Deeney alisema .

Timu ambazo zinashiriki ligi kuu ya Uingereza zimeanza kurejelea kufanya mazoezi kama njia ya kujianda kukamilisha msimu huu baada ya kusitishwa kutokana na janga la Corona.