Kocha wa timu ya Ubelgiji Martinez atia mkataba mwengine hadi 2022

MATINEZI (1)
MATINEZI (1)
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji Robert Martinez ametia kandarasi nyingine ya miaka 2 hadi 2022, taarifa ambazo zimethibitishwa na shirikisho la soka la taifa.

Mkufunzi huyo wa miaka 46 alichukua hatamu hiyo mwaka 2016 na kuwaongoza kufuzu hadi mashindano ya kombe la dunia la mwaka 2018.

Ameongoza Ubelgiji kwa mechi 43 akishinda 34, kwenda sare mara 6 na kushindwa mechi tatu  na kuiwezesha timu hiyo ya kitaifa kushikilia nambari moja katika orodhesho la FIFA.

Martinez alianzia taaluma yake ya ukufunzi katika klabu ya Swansea mwaka 2017 , akajiunga na Wigan Athletics ambapo alishinda taji la FA dhidi ya Man City.