Wachezaji wengi wameathirika Kisaikolojia - Michael Bennett

Huku shughuli zote za michezo zikiwa zimesitishwa katika baadhi ya mataifa ulimwenguni, huenda asilimia kubwa ya wachezaji wameathirika kisaikolojia ama wanakumbwa na mzongo wa mawazo.

Haya ni kulingana  na  mkurugenzi wa shirika la wachezaji Uingereza PFA Michael Bennett .

Ameongeza kuwa wachezaji wengi hawana ufahamu wa iwapo watarejelea shughuli hiyo tena.

“They don’t know if they’re going to go back to football, they don’t know if the football season will start again, they’re not sure what’s going on,” amesema Bennet.

Maswali mengi yamekuwa yakiibuliwa haswa kuhusiana na usalama wa wachezaji wakati ambapo ligi tofauti zimetangaza mpango wa kurejelea hali yake ya kawaida.

Vilabu vile vile vimeandikisha hasara kubwa kutokana na hatua ya kusitisha ligi huku vilabu vingine vikilazimka kuwarudishia mashabiki wake vyeti  kutokana na hatua ya michezo kuanza kusakatwa bila ya mashabiki.

Miongoni mwa wachezaji ambao Bennet amesema pia wanakumbwa na shida ya kisaikolojia kwa sasa ni wale ambao hawana ufahamu iwapo kandarassi zao zitarefushwa au la.