Odion Ighalo kusalia Old Trafford hadi Januari 2021- Sky Sports

3yV_Rw72.jfif
3yV_Rw72.jfif
Klabu ya Manchester United imeafikiana na Shanghai Shenua ili kuongezea mkataba wa  mshambulizi Odion Ighalo hadi Januari 2021, shirika la Sky sports limeripoti.

Ighalo alijiunga na United kwa mkopo akitokea ligi ya Uchina na ambapo kufikia sasa ametinga nyavuna magoli manne katika mechi nane ambazo amechezea mashetani wekundu hao wa Old Trafford.

Mkataba baina ya Ighalo na waajiri wake Shanghai Shenua unatazamiwa kuisha Disemba 2022 huku pakiwepo na matumaini ya kuongezea mkataba huo hadi mwaka 2024.

Kutokana na taarifa hizo sasa Ighalo anatazamiwa kukosa kushiriki mechi za Chinese Super league baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana kuongeza muda wake wa kuhudumu ndani ya United.