Kisa cha kwanza cha corona charipotiwa katika Kambi ya klabu ya Tottenham

diNBNTMt.jfif
diNBNTMt.jfif
Tottenham Hotspur imethibitisha kuwa mtu mmoja katika klabu hiyo amepatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo kama njia ya kujiandaa kwa ligi inayotazamiwa kurejea Juni 17.

Klabu hiyo sasa imesema kuwa mgonjwa huyo atatengwa kutoka kwa wengine ili kupunguza maambukizi japo hawakutoa jina lake halisi.

Tangu kurejelewa kwa mazoezi na timu zinazoshiriki ligu kuu ya Uingereza, waachezaaji 12 kufikia sasa wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo hatari.

Ligi kuu ya Uingerteza ilisitishwa Machi baada ya baadhi ya Mameneja kuambukizwa virusi hivyo.