Mwanga mpya! Uwanja wa Nyayo wavutia baada ya kukarabatiwa

Nyayo-Stadium-spots-a-new-magnificent-look
Nyayo-Stadium-spots-a-new-magnificent-look
Kamati ya michezo katika bunge la kitaifa imeelezea furaha yao kuhusiana na sura mpya ya uwanjwa wa michezo nchini wa Nyayo.

Uwanjwa huo ambao ndio wa pili kwa ukubwa nchini umekuwa ukikarabaitiwa kuanzia 2017 na kufikia sasa asilimia 95 ya ukarabati huo umekamilika.

Kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti na mbunge wa Machokos Town Victor Munyaka, ilizuru katika uga huo ambapo walisifia pakubwa hatua ambazo zimepigwa na aliyepewa zabuni ya kuukarabati.

“The committee is pleased with the progress of the works here (Nyayo) and we are very pleased that in a week’s time the contractor will be handing over the facility so that the stadium will be ready for use as soon as sporting actions resumes when Covid-19 is contained,” amesema Munyaka.

Pia mwenyekiti wa Sports Kenya Fred Muteti na meneja mtendaji Pius Metto walisifia pakubwa utendakazi wa aliyepewa kandarasi ya kuutengeneza uwanja huo.

“Through the support we got of the budget we have been able to complete this stadiuma nd we are also in the process of finalizing works at Kasarani. We are prepared now and with the fund I don’t think we will have any further delays,” alisema Muteti.

 Muteti amesema kuwa serikali pia itaanza kuangaazia viwanja vingine nchini ili kuvifanyia marekebisho.

Wakati uo huo, Munyaka amesema yeyote atakayepatikana na hulka za kuharibu viwanja ambavyo vimekuwa vikikarabatiwa nchini atachukuliwa hatua za kisheria.

“For this good investment to be protected, we need proper investment on crowd control and security within the stadium and its environs so that we don’t have hooligans accessing any event within the stadium,” aliongezea  Munyaka.

Tayari eneo la kukalia kwa watu mashuhuri katika uwanja wa Nyayo umekamilika huku maeneo ya wachezaji kuvalia nguo pia ikiwa na mwanga mpya ..