Arsenal Yakung'utwa magoli 3 na Man City

Eavl9llWsAI37tq.jfif
Eavl9llWsAI37tq.jfif
Matumaini ya Arsenal ya kumaliza miongoni mwa vilabu nne bora ilipata pigo kufuatia ushindwa wa 3-0 kwa Man City ugani Etihad.

Mechi hiyo ya Jumatano, Juni 17 usiku, ilikuwa siku ya pili tangia Ligi Kuu kurejea baada ya kusitishwa kwa wiki kadhaa.

Huku Man City wakiwa tayari nje ya kinyang'anyiro cha kutwaa taji, Arsenal ndio walikuwa wakikaza kamba ili kujipatia tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Hata hivyo, hayo yalitibuka, huku Gunners wakikumbana na majeraha mawili kwa mpigo dakika chache kabla ya mechi hiyo.

Granit Xhaka ndiye alikuwa wa kwanza kuondoka uwanjani dakika tano kabla ya mechi kuanza baada ya kupata jeraha la mguu.

Nafasi yake ilichukuliwa na Dani Ceballos ambaye alijiunga na David Luiz kutoka kwenye benchi dakika 22 baada ya Pablo Mari kupata jeraha.

Lakini kushirikishwa kwa Luiz ndio ilikuwa mwanzo wa mikosi ya Arsenal, huku utepetevu wa difenda huyo Mbrazil ukimruhusu Raheem Sterling kufunga bao la kwanza kabla ya muda wa mapumziko.

City iliwatinga bao lao lingine dakika nne baada ya awamu ya pili kuanza kupitia kwa Kevin de Bruyne ambaye alifunga bao baada ya Luiz kusababisha penalti.

Kisa hicho kilimshuhudua difenda huyo wa zamani wa Chelsea kulishwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Riyadh Mahrez.