Komesha Ubaguzi! Wacheza wapiga magoti kukomesha ubaguzi wa rangi

download-1 (1)
download-1 (1)
Wachezaji wa timu za Aston Villa na  Sheffield United pamoja na muamuzi Micheal Oliver walipiga magoti chini kabla ya kuanza kwa mchezo kama njia ya kukomesha ubaguzi wa rangi chini ya kauli mbiu Black Lives Matter.

Ligi kuu ya Uingereza ilirejea hiyo jana baada ya siku 100 kutokana na mkurupuko wa corona na timu mbalimbali zilikubaliana kutumia dakika moja ya kupinga ubaguzi wa rangi ambao umekuwa ukishuhudiwa katika mataifa ya kigeni.

Majina ya wachezaji katika sare zao rasmi, yalioondolewa na kuandika Blac Lives Matter kama njia ya kukashifu tukio ambapo raia mweusi George Floyd aliuawa na askari wa kizungu Amerika, tukio lililosababisha maandamano katika mataifa mengi.

Kulishuhudiwa pia kimya cha dakika moja kama heshima kwa watu waliopoteza maisha yao kutokana na virusi vya corona.