Lampard akana kuwa na mipango ya kumuuza Kante

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard amekana kwamba klabu ya Chelsea itafadhili uhamisho wa mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, na beki wa kushoto wa Leicester na England Ben Chilwell, 23, kwa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 29, mwisho wa msimu huu . (Guardian)

Lampard amtaka mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 22, kujiimarisha kufuatia usajili wa mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 24, kutoka RB Leipzig. (Metro)

Manchester City iko tayari kumuchailia winga wa Ujerumani Leroy sane 24 kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa kandarasi yake iwapo klabu ya Ujerumani ya Bayern Munchen itaongeza thamani yake ya pauni milioni 30.. (Independent)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil anataka kukamilisha kandarasi yake akiichezea Arsenal licha ya kwamba The Gunners inataka kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 , ambaye analipwa kitita cha 350,000 kwa wiki mwisho wa msimu huu kutokana na sababu za kifedha. (ESPN)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, anasema kwamba anataka kushinda mataji zaidi akiichezea Chelsea na kwamba kuwasili kwa Warner kutampa changamoto zaidi . (Guardian)

Roy Hodgson anasema kwamba klabu ya Crystal Palace itafanya ujinga kupumzika na kujisahau na kufikiria hakuna timu itakayowasilisha ombi la kutaka kumnunua winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha mwisho wa msimu huu kutokana na athari za kifedha zilizosababishwa na Covid-19.. (London Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Papa Gueye, 21, amekubali kujiunga na Watford baada ya kandarasi yake katika klabu ya Le havre kukaribia kukamilika msimu huu , lakini wakala wake anasema kwamba hataki mchezaji huyo kujiunga na Watford na Arsenal tayari imempatia ofa huku nayo Marsaile ikiwa miongoni mwa klabu ambazo zinamnyatia. (Le Phoceen, in French)

Steve Bruce anasema kwamba amechoka kusikiliza madai kwamba kazi yake ipo hatarini kama mkufunzi wa Newcastle iwapo uuzaji wa klabu hiyo utakamilika. Mkufunzi Mauricio Pochettino na Rafael Benitez wamehusishwa na klabu hiyo. (Telegraph)

Atletico Madrid ilikataa dau la $136m kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 20, kutoka klabu ya Uingereza kabla ya mlipuko wa corona.. (Goal)

-BBC