Nne Bora : Juhudi za Arsenal zapata pigo kubwa baada ya kunyukwa 2-1 na Brighton

_113003348_gettyimages-1221138955
_113003348_gettyimages-1221138955
Juhudi za Arsenal za kumaliza katika nafasi ya nne bora kwenye ligi ya primia zilipata pigo kubwa baada ya kunyukwa mabao  2-1 na Brighton.

Neil Moupey alifunga goli la ushindi katika dakika za mwisho baada ya Luke Dunk kusawazisha goli la ufunguzi la Nicolas Pepe katika kipindi cha pili.

Katika mechi nyingine Wolves ilisalia katika nafasi ya tano na alama sawia na Manchester United baada ya kuilaza West ham 2-0, huku Leicester ikitoka sare ya 1-1 na Watford.

Atletico Madrid ilipanda hadi nafasi ya tatu kwenye jedwali ya La liga baada ya kuinyuka Valadolid 1-0 kupitia goli la Pirez Vitolo.

Katika mechi zingine zilizopigwa Jana, Athletic Bilbao ililaza Real Betis 1-0 huku Getafe na Eibar zikitoka sare ya 1-1.

Gwiji wa tenisi Serena Williams yuko tayari kucheza bila ya mashabiki kwenye michuano ya US Opens inayotarajiwa kuanza Agosti tarehe  31.

Haya yanajiri licha ya wachezaji kadhaa wenye tajriba ya juu akiwemo Simoa Halep kudai hawatacheza kutokana na masharti iliyowekwa na wasmamizi.

Iwapo Mmarekani huyo atanyakua taji hilo, atafikia rekodi ya grand slam ya mataji 24 inayoshikiliwa na mchezaji wa Australia,  Margaret Court.

Kwingineko, Mwanaridha wa masafa marefu Japheth Kipkorir atatumikia marufuku ya miaka minne baada ya kupatikana na kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli.

Hayo ni kwa mujibu wa tume la kupambana na utumizi wa dawa duniani WADA. Kipkorir ambaye alikua akichunguzwa pia ata nyang'anywa mataji yote aliyoshinda tangu mwaka wa 2013.