Jose Mourinho asajili ushindi baada ya mechi 8

Tottenham Hotspur walisajili ushindi wao wa kwanza baada ya michezo minane kupitia kwa magoli yaliyofungwa na Harry Kane na la kujifunga kupitia mchezaji Tomas Soucek.

Soucek alijifunga baada ya mchezaji wa Spurs Giovanni Lo Celso kupiga mkwaju wa kona ambao ulitumbukia katika nyavu za Westa Ham baada ya mpira kumgonga Soucek mguuni.

Son alitangulia kufunga goli kabla yaa kipindi cha kwanza kutamatika japo likafutiliwa mbali na muamuzi .

Akizungumza baada ya mchezo huo, mkufunzi wa West Ham David Moyes alisema goli la kwanza la Tottenham lilistahili kufutiliwa mbali baada ya Son kunawa mpira.

"I've only just seen it, and I can't believe they've ruled that as a goal. Any handball is disallowed? That's the rule. Who is on VAR tonight? Not very good eh?” Moyes .

Ushindi huo sasa unaipeleka timu ya Spurs kuwa na alama 45, alama sita tu kufuzu katika mashindano ya mabingwa Ulaya.

Kwa upande wao West Ham wanasalia katika nafasi ya pili mwisho wa ligi huku tofauti ya magoli ikiwatenganisha na wenzao Haddersfiled.