Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier kutetea kiti chake mwezi Agosti

images (4)
images (4)

Mwenyekiti wa klabu ha Gor Mahia Ambrose Rachier atatetea kiti chake katika kura klabu zijazo tarehe nane Agosti.

Rachier ambaye ameongoza mabingwa hao wa KPL kwa zaidi ya mwongo mmoja, alikua ametishia kutosimama tena lakini alibadili kauli yake. Viti vinne vitawaniwa katika kura hizo zitakazofanyika mtandaoni, zikiwemo mwenyekiti msaidizi, mweka hazina na kati u mtendaji.

Wilson Kipsang ata kata rufaa katika mahakama ya spoti duniani, kutokana na marufuku ya miaka minne aliyopewa na shirkisho la riadha duniani.

Kipsang ambaye hapo awali alishikilia rekodi ya marathon duniani anadai hajawahi kutumia dawa za kusisimua misuli na amedai anabaguliwa tuu kwa kuwa yeye ni mwafrika. Kipsang alipatikana na kosa la kukiuka kanuni za utumizi wa dawa na pia kukwepa kupimwa.

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo na Paolo Dybala walifungia Juventus na kuisadia kuinyuka Torino 4-1, huku wakikaribia kunyakua taji la tisa mfululizo la ligi ya Italia.

Wapinzani wao wa Karibu Lazio nao walipokea kichapo cha mbwa baada ya kunyukwa 3-0 na AC Milan. Juve sasa inaongoza jedwali la serie A alama saba mbele ya Lazio huku zikiwa zimesalia mechi nane.