Chelsea yawalaza Crystal Palace mabao 3 kwa 2 na kuchukua nafasi ya tatu kwenye jedwali

Ni mechi ambayo ilikuwa imesubiriwa sana na mashabiki wa Chelsea. Chelsea iliilaza timu ya Crystal Palace mabao 3 kwa 2. Chelsea wanapigania kuhifadhi nafasi yao katika timu nne bora katika ligi kuu nchini Uingereza.

Chelsea waliingia katika mechi hiyo bila huduma ya wachezaji watatu wa kutegemewa ikiwemo N'Golo Kante, Mateo Kovacic na Fikayo Timori.

Hata hivyo, kikosi hicho kilifaulu kustahimili mashambulizi ya Palace na kutwaa ushindi mkubwa ugenini.

https://twitter.com/ChelseaFC/status/1280758012630773761

Wilfried Zaha alifungia Eagles bao na kupiga nduki yenye ustadi katika kipindi cha kwanza  wakitawala mchezo huo huku wakitafuta bao lingine la kusawazisha.

Hata hivyo, walipata pigo kubwa dakika ya 71 baada ya Tammy Abraham kuungana na Loftus-Cheek kugeuza matokeo kuwa 3-1 kabla ya Christian Benteke kufungia wenyeji bao lingine.

Licha ya kuwa kifua mbele, mabarubaru wa Frank Lampard walikabiliana na presha ya Palace dakika za lala salama za mechi kushikilia ushindi wao.

Ushindi huo unawaweka katika nafasi ya tatu kwenye jedwali wakiwa na pointi 60, pointi mbili mbele ya Leicester.