Tottenham yawalaza Arsenal mabao 2 kwa 1 huku Gunners ikichukua nafasi ya tisa katika jedwali ya ligi kuu

Ni mchuano ambao wengi walitabiri na kusema Gunners wataibuka washindi. Tottenham waliwapa Arsenal kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Tottenham Hotspur wameongeza nafasi yao ya kushiriki mtanange wa Bara Ulaya kufuatia ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Arsenal katika debi ya London.

Mabao kutoka kwa Son Heung-Min na Toby Alderweireld yalitosha Spurs kusajili ushindi mkubwa nyumbani siku ya Jumapili, Julai 12.

https://twitter.com/MikelArt3ta/status/1282365905180254209

Mabao hayo mawili yalipelekea bao la kwanza la Alexander Lacazette kuwa la kufutia machozi huku Gunners wakihangaika kutafuta bao la kusawazisha katika mechi hiyo. Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Jose Mourinho na Mikel Arteta katika debi ya London huku wakufunzi hao wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa wametiwa adhabu.

Spurs walikuwa kwenye mchakato wa kuwarejeshea mashabiki wao matumaini kufuatia matokeo yao mabovu tangu kurejea kwa ligi hiyo.

Lakini Gunners ndio walitingisha wavu wa kwanza baada ya Alexander Lacazette kuvurumisha kombora kali lililompita Hugo Lloris na kufanya matokeo kuwa 1-0.

Matokeo hayo yaliwashuhudia Spurs wakisonga mbele ya Arsenal katika nafasi ya nane na pointi 50 huku vijana wa Mikel wakishuka hadi nafasi ya tisa na matumaini yao ya kushiriki mashindano ya bara Ulaya yakizimwa