FA Cup: Wanabunduki walipua Manchester City na kujikatia tikiti ya fainali

Arsenal
Arsenal
Ndoto ya Manchester City ya kuteteta kombe la FA ilizimwa waliponyukwa mabao 2-0 na Arsenal katika mechi ya nusu fainali ugani Wembley.

Mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang kunako kila kipindi yalitosha kuwapa ushindi vijana wa Mikel Arteta na kumpa ushindi wake wa kwanza dhidi ya Pep Gurdiola tangu kuondoka Etihad. The Gunners watakabana na aidha Chelsea au Manchester United ambao wanachuana katika nusu fainali ya pili usiku wa leo.

Meneja wa Manchester City Pep Gurdiola anasema Arsenal walistahili kushinda nusu fainali ya kombe la FA jana kufuatia mchezo wao mbaya. The gunners waliwanyuka City mabao 2-0 ushindi wao wa kwanza dhidi ya mabingwa hao watetezi katika mechi tisa. Guardiola pia anaamini kuwa aliyekuwa msaidizi wake Mikel Arteta atashinda mataji ugani Emirates, iwapo atapata usaidizi.

Tukirudi nchini, soka na raga zitachukua muda zaidi kuregelewa humu nchini, kufuatia ongezeko la maambukizi ya covid-19. Katibu wa afya Rashid Aman anasema wanatathmini kufungua michezo isiyo ya kugusana, ikifuatia iliyo na mgusano kidogo na kisha yenye kugusana kabisa kama vile raga na soka.

Jopokazi lililoundwa na waziri wa michezo Amina Mohammed kushauri kuhusu kuregelewa kwa spoti humu nchini, litawasilisha ripoti yake hivi karibuni.