Nataka kukuza soka kutoka mashinani na kutoa mafunzo zaidi kwa refarii- Tom Alila Azungumza

Tom Alila ambaye anafahamika sana kwa sasa anataka kuwania kiti cha urais katika sekta ya soka, huku akizungumza na radiojambo Alila alisema kuwa anataka kukuza mchezo wa kandanda kutoka mashinani.

Alila amekuwa na rekodi njema kutoka awali katika sekta ya soka.

"Nitatoa mafunzo zaidi kwa refarii na hata kuleta usawa katika malipo ya wanakandanda wa kike na wakiume, pia nataka kushirikiana na serikli ya kaunti kutoa msaada kwa wanakandanda ili waweze kujisimamia maishani mwao.

Pia nitaongeza muda wa KPL, na hata kutoa mafunzo zaidi kwa makocha na wala si refarii pekeyao." Alizungumza Alila.

Alila akizungumzia uchaguzi wa sekta ya soka alisema kuwa katika uchaguzi mkuu watazingatia jinsi rais ametekeleza ahadi yake aliyoahidi atatekeleza.

Pia alisema wakati wa uchaguzi wapiga kura wanapaswa kusema ukweli na bila kuharibu jina la