Champions league : Lyon yalaza Manchester City 3-1

IMG_20200816_090728
IMG_20200816_090728

Olympic Lyon ya Ufaransa ilifunga miamba wa Uingereza Manchester City 3-1 katika robo fanali ya klabu bingwa bara Ulaya na kufuzu kwa nusu fainali. Kevin De Bruyne alisawazishia City kunako dakika ya 69  baada ya Maxwel Cornet kuwapa Lyon Uongozi katika kipindi cha kwanza.

Mousa Dembele alivunja nyoyo za wawingereza kwa mabao mawili katika dakika ya 79 na 87. Lyon itapambana na Bayern Munich huku RB Leipzig ikipiga dhidi ya PSG katika nusu fainali ya pili.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michuno hii timu mbili za Ufaransa PSG na Lyon kufuzu kwa nusu fainali.

Newcastle wananuia kumsajili mlinzi wa  Manchester United Chris Smalling huku kocha Steve Bruce akiwania kudhibiti ngome yake ya ulinzi.

Smalling anapigiwa upatu kujiunga na Newcastle baada ya kuwa na muda mzuri sana nchini Italia akichezea Roma katika ligi ya  Serie A. Miungereza huyo mwenye umri wa miaka 30 amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na United.