Hongera:Brigid Kosgei ashinda mbio za London Maranthon

Mwanariadha Brigid Kosgei hii leo ameshinda mbio za London Marathon, Kosgei alikimbia mbio hizo na kukamilisha kwa muda wa 2:18:58 huku akiwashinda wanariadha wenzake 18 katika mbio ambazo ziliwashirikisha mabingwa wa riadha.

Alipokuwa amekariba kukamilisha kilomita saba kwenye barabara zenye unyevunyevu katika jiji la London, mwanariadha huyo alikuwa na tabasamu kubwa usoni na alifahamu fika angeibuka mshindi.

Bingwa wa dunia Ruth Chepng'etich alimaliza wa tatu baada ya kupitwa na Mmarekani Sarah Hall zikibakia 500m pekee kufika utepeni.

Mashindano hayo ya 30km yalifanyika bila ya kuwapo mashabiki kwa sababu ya tahadhari zilizowekwa kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Kufuatia ushindi huo wa dhahabu, Kosgei amepongezwa na watu mbalimbali wakiwamo Naibu Rais William Ruto, Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga miongoni mwa Wakenya wengine wa matabaka mbalimbali.

Viongozi mbalimbali wamempongeza Kosgei ikiwemo kinara wa ODM Raila Odinga na naibu rais William Ruto.