Mwanakandanda Sadio Mane apatikana na virusi vya corona

Sadio Mane
Mchezaji wa timu ya Liverpool Sadio Mane amepatikana na virusi vya corona huku akiwa mchezaji wa pili katika klabu hicho kuambukizwa virusi hivyo.

Mane,28 ambaye ni mshambulizi wa timu hiyo hataweza kusafiri wikendi hii hadi maeneo ya Villa ili kumenyana na timu ya Aston Villa.

Nduru za habari zinaarifu ya kwamba Mane tayari amejitenga ili kuthibiti kusambaa kwa virusi vya corona, pia iliaminika kuwa mchezaji huyo anaendelea vyema.

"Sadio Mane amepatikana na corona lakini amejitenga huku akifuata kanuni za wizara ya afya, hata hivyo kama vile Thiago Alcantara,wachezaji wa liverpool watazidi kufuata kanuni za covid-19 huku mane akijitenga kwa muda unaofaa."

Haya yanajiri siku chache baada Thiago Alcantara kupatikana na virusi hivyo.