Watu wamekuwa wakikula pesa za soka na ligi Nairobi-Tom Alila

Muhtasari

•Watu waache kuwatisha wawakilishi ili wasipatane na wawaniaji viti

•Wamekuwa wakila pesa za ligi na soka kwa muda mrefu

•Mwenye tumesimama naye ni kama handbag ya rais ya kukula pesa

Tom Alila

Jumamosi ni siku ambayo imesubiriwa sana na wachezaji na wawaniaji kiti cha urais sekta ya  soka humu nchini huku wakipiga kura siku hiyo katika uwanja wa safari park,miezi michache iliyopita akizungumza na radiojambo Tom Alila alisema kuwa atawania kiti hicho huku akibadilisha msimamo wake na kutaka kuwa mwanachama wa soka.

"Watu wengi wamekuwa wakikula pesa za soka huko Nairobi, sitataja jina lakini wengi wamesimama kuwania kiti cha urais cha soka

Kila mtu si lazima awe wa kaunti hiyo ili awanie kiti cha urais,mwenye tumesimama naye ni kama 'handbag' wa kukula pesa za ligi

 

Nimekuwa katika shirikisho kwa miaka mingi na nimefanya mambo mengi, watu wanapaswa kuacha kutisha watu ili wasiwapigie baadhi ya watu kura." Alisema Alila.

Alila alisema kuwa ataungana na gavana Sonko ili kuendeleza soka mbele na kuhakikisha kuleta maendeleo katika sekta ya soka.

"Katika kinyang'anyiro cha jumamosi tunapaswa kujitokeza na kupiga kura, ili tufanyie kazi watu wa Nairobi

Hakuna haja ya kuwaficha wawakilishi, wamekuwa wakipigiwa simu na kutishiwa maisha wasipatane na watu fulani

Kiongozi anapaswa kuwa  na kura 87 na Nairobi wana kura mbili tu, mimi nikipiga hesabu kwa sasa nina kura zaidi ya 40 kama wawakilishi hawatatishiwa maisha."

Tom alisema kuwa lazima waongee na viongozi na wawakilishi kwa unyenyekevu ili wawapigie kura na kuwa wawache kuwatishia watu maisha.

"Ausi ni handbag ya rais wa kutishia watu maisha ambayo ametoka nayo kariobangi sharks."

Maneno yake yalijiri siku chache baada ya Macharia kusema kwamba Alila ameshindwa kutekeleza majukumu yake katika eneo la Nairobi.