Nick Mwendwa ashinda katika uchaguzi wa FKF

Muhtasari
  • Nick Mwendwa ashinda kuwa rais wa FKF kwa kura 77
nick mwendwa
nick mwendwa

Nick Mwendwa ameshinda katika kinyang'anyiro cha uaniaji urais wa Football Kenya Federation hii ni baada ya kuwashinda wenzake wanne kwa kura 77 katika uchaguzi ulioandaliwa katika eneo la Kasarani.

Aliyekuwa amemfuata ni aliyekuwa afisa mkuu wa timu ya Gor Mahia Lordvick Aduda aliyejifunga na kura tano.

Aliyekuwa naibu mkurugenzi mkuu wa FKF Hebert Mwachiro alikuwa katika nafasi ya tatu na kura tatu, huku wawaniaji kiti hicho Boniface Osano na Dan Mule hawakujinyakulia kura ata moja.

Katika kamati ya utendaji wa kitaifa wa FKF  mwenyekiti  wa kamati ya maandalizi ya mechi za kitaifa Michael Ouma alimshinda Tom Alila katika kiti cha mkoa wa Nairobi.

Ouma alifanya kazi kama mwenyekiti kwa miaka minane na kumshinda Alila kwa kura 59 huku Alila akinyakulia kura 25 huku Isaac Macharia akiwa na kura moja katika nafasi ya tatu.