Sonko anahitaji kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini, Mahakama yaambiwa

sonko
sonko

Daktari wa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko, anasema anahitaji kusafiri kwenda Afrika Kusini kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha nyonga.

Ripoti iliyowasilishwa na Daktari Esther Wekesa kutoka hospitali ya Kenyatta inasema upasuaji huo unahitaji kufanywa haraka iwezekanavyo kwani asipotibiwa huenda akakumbwa na matatizo zaidi ya kiafya.

Walakini, Plank hawezi kusafiri kuja Kenya kwa sasa na anasema atamkagua Sonko huko Johannesburg. "Nimezungumza na Dk Plank kwa simu na barua pepe juu ya kuchukua kesi hiyo lakini hajasafiri hadi Kenya katika miaka 2 iliyopita na anasema hatakuja wakati wowote hivi karibuni," inasoma ripoti hiyo.

Washukiwa wengine wawili ambao walikamatwa na Sonko katika kesi ya ugaidi wameachiliwa bila masharti.

Wakili Danstan Omari wa upande wa utetezi aliambia korti huko Kamiti kwamba wawili hao wamepata Covid-19 wakiwa kizuizini.

Omari aliambia korti kuwa wawili hao ambao wamekaa kizuizini kwa siku 26 walikuwa wakiteswa kwa kuwa washirika wa Sonko. Upande wa mashtaka uliiambia korti kuwa wamehitimisha uchunguzi juu ya wawili hao na hawatawashtaki.

Kesi hiyo itatajwa mnamo Machi 3 wakati hakimu wa kesi hiyo ambaye hakuwa karibu siku ya Ijumaa atarejea kutoa maagizo juu ya ripoti ya matibabu iliyotolewa kortini.