Harambee Stars yailaza Sudan Kusini katika mechi ya kirafiki

rupia harambee stars
rupia harambee stars

Harambee Stars iliifunga Sudan Kusini 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa jana kwenye ukumbi wa Nyayo.

Elvis Rupia aliifungia Kenya bao la pekee katika dakika ya 76, baada ya kutoka sare tasa katika kipindi cha kwanza lakini, Stars ilishikilia ushindi.

Kenya itacheza na Tanzania kesho, na Jumatano katika mechi za kirafiki jijini Nairobi. Misri inatarajiwa kusafiri humu nchini mnamo Machi 22, kumenyana na Stars katika mechi za  Group G za kufuzu AFCON 2020.

Kenya Harlequins waliwanyuka Impala 27-20 katika michuano ya raga ya Ngong road derby, Kenya Cup ilipoingia wiki ya tatu jana. Wakati huo huo Mwamba walinyukwa 17-24 na Blak Blad, huku Menengai Oilers wakiwabandua Top Fry Nakuru 21-20 katika mechi ya kusisimua ya derby ya Nakuru. Mabingwa KCB, Kabras Sugar na Strathmore walipumzika na wataregea wikendi ijayo, msimu utakapoingia wiki ya nne.

Bingwa wa mbio za mita elfu tano kwa kinadada Hellen Obiri aliibuka mshindi katika mkondo wa pili wa mbio za mita elfu 10 za Athletics Kenya Track and Field hapo jana katika uwanja wa Kasarani.

Obiri alikimbia kwa dakika 31 na sekunde 24 na kumshinda Eva Cherono, na Vicky Chepng’eno walioibuka katika nafasi ya pili na tatu mtawalia. Katika mbio za wanaume Mark Otieno aliibuka mshindi na kumpiku Ferdinand Omanyala na Tazana Kamanga.

Arsenal itapambana na Tottenham katika London derby ugani Emirates, huku pande zote mbili zikiwania ushindi.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta hana majeruhi wowote wapya naye Jose Mourinho akitarajia Harry Kane kurejea kutoka kuuguza jeraha.

Kwingineko Leicester City wanachuana na  Sheffield United wanaovuta mkia, huku Manchester United wakiwaalika West Ham ugani Old Trafford katika kinyangányiro cha nne bora. Anthony Martial, Marcus Rashford na Edinson Cavani hawatakuwepo kwenye kikosi cha United kwani wanauguza majeraha.