Michael Olunga hatimaye azungumza baada ya kupatikana na corona

Muhtasari
  • Mwana kandanda wa timu ya Harambee Stars Michael Olunga amezungumza baada ya kudaiwa kuwa na virusi vya corona alipokuwa nchini Togo
Michael Olunga
Image: Harambee Stars

Mwana kandanda wa timu ya Harambee Stars Michael Olunga amezungumza baada ya kudaiwa kuwa na virusi vya corona alipokuwa nchini Togo.

Olunga alikuwa ameenda katiia mchuano wa Africa Cup of Nation qualifiers, katii ya timu ya Harambee Stars na Togo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Olunga alikuwa na haya ya kusema,

 

"Wakati tu baada ya mawingu ya dhoruba kupita, wakati yote ni kimya na bado, unapata amani na utulivu. 🙏🏾," Aliandika Olunga.

Siku ya Jumatatu Ripoti ziliarifu kwamba wanakandanda 4 wa timu ya Harambee Stars walipatikana corona baada ya kuwasili Togo.

Wachezaji hao ni pamoja na Michael Olunga, Joash Onyango, Lawrence Juma na Ian Otieno, maafisa wakuu wa FKF bado hawajatoa taarifa kuhusu madai hayo.

Licha ya wanne hao kukosa uwanjani Harambee iliwalaza Togo mabao 2 kwa 1