LIGI KUU UINGEREZA

EPL 2021: Jumapili ya drama Uingereza

Liverpool na Chelsea zahitimu kucheza ligi kuu ya Ulaya, Hakuna ligi ya bara la Ulaya kwa Arsenal msimu ujao.

Muhtasari

•Manchester City, Manchester United, Liverpool na Chelsea zitashiriki kwenye ligi ya mabingwa katika msimu wa 2021/22

•Arsenal itakoseka kushiriki kwenye ligi za bara la Ulaya kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Gareth Bale asherehekea kufunga
Gareth Bale asherehekea kufunga
Image: HISANI

Msimu wa 2020/21 wa ligi kuu ya Uingereza(EPL) ulifika tamati siku ya Jumapili huku michuano kumi ikichezwa.

Matokeo makubwa yaliandikishwa huku mabao mengi yakifungwa lakini kunazo mechi zilizokuwa zinaangaziwa sana na mashabiki wengi kwani zingeamua klabu zipi zingecheza kwenye ligi ya mabingwa nay a Europa msimu ujao.

Klabu ya Liverpool  iliipiga Crystal Palace 2-0 na kujihifadhia nafasi kwenye nne bora ikiandikisha alama 69 huku Leicester ikipigwa na Tottenham 2-4 na kuanguka hadi nafasi ya tano na alama 66 na kuachia Chelsea nafasi ya nne ikijinyakulia alama 67 baada ya kupigwa na Aston Villa 2-1.

Manchester City, Manchester United, Liverpool na Chelsea zitashiriki kwenye ligi ya mabingwa katika msimu wa 2021/22 baada ya kuchukua nafasi 1,2,3,4 mtawalia.

Jedwali la EPL
Jedwali la EPL
Image: HISANI

Arsenal itakoseka kushiriki kwenye ligi za bara la Europa kwa mara ya kwanza ndani ya miongo miwili baada ya kumaliza nambari nane na pointi 61. Usindi wa Spurs dhidi ya Leicester ulisaidia timu hiyo kuchukua nafasi ya saba na kwa hivyo kuhitimu kushiriki ligi ya muungano wa Europa(Conference League).

Leicester na Westham zitashiriki kwenye ligi ya Europa baada ya kumaliza nambari 5 na 6 mtawalia na pointi 66 na 65.

Fulham, Westbrom na Sheffield United hazitakuwemo kwenye ligi ya EPL msimu ujao baada ya kushushwa ngazi kuenda ligi ya Championship.