EPL: Mlinzi Ruben Dias atuzwa kama mchezaji bora wa msimu uliopita

Ruben Dias na Pep Guardiola
Ruben Dias na Pep Guardiola
Image: Manchester Evening news

Mlinzi wa Manchester City Ruben Dias ametuzwa kama mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno pia alichaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka na Chama cha Waandishi wa Soka mnamo mwezi Mei.

Kocha wa City Guardiola aliteua kama meneja bora wa Ligi Kuu msimu huu, kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne. Phil Foden ndiye alinyakua tuzo la mchezaji bora asiyezidi umri wa miaka 23.

Ufuatao ni mkusanyiko wa habari za spoti humu nchini;

Tusker hapo jana walifuzu kwa robo fainali ya michuano ya FKF Cup ya mwaka 2021, kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya daraja la chini Luanda Villa katika uwanja wa Ruaraka. Bao la pekee la wanamvinyo hao liifungwa na Henry Meja kunako dakika ya 41. Kwingineko Bidco pia walijikatia tikiti kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya AFC Leopards, huku Equity wakiwabandua  Vegpro 2-1. 

 Michuano ya FKF betway Cup inaingia raundi ya 16 bora hii leo, huku KCB na Kariobangi Sharks wakicheza jioni ya leo. AFC Leopards watawaaika Bungoma Supers Stars, Gor Mahia watakabana na Mara Sugar huku Ulinzi Stars wakichuana na City Stars.  Mabingwa wa zamani Bandari watamaliza udhia dhidi ya Sigalagala TTI .

Mbio za marathon za Eldoret City zinafanyika hii leo katika kaunti ya Uasin Gishu. Mbio hizi zitawajumuisha wanariadha kadhaa wa hadhi ya juu, watakaokuwa wakiwania kushinda mataji, katika mbio hizo, mojawapo ya mbio za kifahari zaidi barani Afrika. Washindi wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watapata tuzo la shilingi miioni 3.5 huku wanariadha 20 wa juu pia wakituzwa.