EURO 2020

Eriksen kuwekwa kifaa cha kudhibiti mapigo ya moyo baada ya kuzirai uwanjani

Kifaa cha ICD kinasaidia kuzuia maafa ya ghafla kwa watu ambao wana mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.

Muhtasari

•Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na raia wa Uholanzi, Daley Blind aliwekwa kifaa hicho baada ya kupatikana na matatizo ya mishipa ya moyo mwaka wa 2019.

Christian Eriksen
Christian Eriksen
Image: Hisani

Baada yakuzirai uwanjani akicheza, mchezaji wa Udenmarki, Christian Eriksen atafanyiwa upasuaji na kuwekwa kifaa cha kufuatilia na kudhibiti mpigo wa moyo.(ICD)

Daktari wa timu ya taifa ya Udenmarki,Morten Boesen, amethibitisha hayo huku akisema kuwa mchezaji huyo amekubalikufanyiwa upasuaji huo.

Kifaa cha ICD kinasaidia kuzuia maafa ya ghafla kwa watu ambao wana mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na raia wa Uholanzi, Daley Blind aliwekwa kifaa hicho baada ya kupatikana na matatizo ya mishipa ya moyo mwaka wa 2019.

Siku ya Jumanne, Eriksen alitoa ujumbe kwa umma kwa mara ya kwanza tangu kuzirai siku ya Jumamosi kwenye mechi dhidi ya Ufini.

Habari yenu nyote. Nawashukuru sana kwa jumbe na salamu zenu nzuri kutoka kote ulimwenguni. Inamaana kubwa sana kwangu na familia. Niko sawa. Hata hivyo, kuna vipimo vitafanyiwa hapa hospitali ila najiskia sawa. Sasa nitashabikia timu ya Udenmarki kwenye michuano ijayo. Tuombee Udenmarki yote” Eriksen aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram huku akipakia picha yake akiwa hospitalini.

Tunamtakia Eriksen heri njema anapoendelea na matibabu.