Mshindi wa WRC Safari Rally 2021, Sebastien Ogier atoa msaada kusaidia miradi miwili Kenya

Ogier ameahidi kutoa msaada wa 1.3Mkwa mradi wa kusaidia watoto kusoma wa Nakuru Children's Project na pesa zingine kama hizo kwa mbuga ya kuhifadhi wanyama ya Ol Pejeta iliyo Laikipia.

Muhtasari

•Kulingana na ujumbe ambao Ogier aliandika kwenye mtandao wa Facebook, ushabiki mkubwa aliopata kutoka kwa Wakenya  na mandhari ya kupendeza aliyoyaona ni mambo ambayo yataishi moyoni mwake milele.

•Ogier aliibuka wa kwanza kwene mashindano ambayo yalitamatika mnamo Juni 27 mjini Naivasha.

Image: FACEBOOK// SEBASTIEN OGIER

Takriban wiki tatu baada na mashindano ya magari ya kidunia, WRC Safari Rally 2021 kukamilika mjini Naivasha, mshindi  Sebastien Ogier hangeficha furaha yake kutokana na yale aliyoshuhudia nchini Kenya.

Kulingana na ujumbe ambao Ogier aliandika kwenye mtandao wa Facebook, ushabiki mkubwa aliopata kutoka kwa Wakenya  na mandhari ya kupendeza aliyoyaona ni mambo ambayo yataishi moyoni mwake milele.

Kufuatia upendo aliopata kwa nchi ya Kenya, Mfaransa huyo ameapa kutoa msaada wa milioni 2.5 kusaidia katika miradi miwili.

Ogier ameahidi kutoa msaada wa 1.3Mkwa mradi wa kusaidia watoto kusoma wa Nakuru Children's Project na pesa zingine kama hizo kwa mbuga ya kuhifadhi wanyama ya Ol Pejeta iliyo Laikipia.

"Nchi hii ya ajabu iko na mahali maalum moyoni mwangu na nataka kurudisha mkono. Masomo ni ufunguo wa maisha mema ya usoni kwa hivyo nataka kusaidia mradi wa Nakuru Children's Project na sh1.3M. Na yafaa tufanye  yote tuwezayo kutunza wanyama pori kwa hivyo nitatoa msaada mwingine wa sh1.3M kwa mbuga ya kuhifadhi wanyama ya Ol Pejeta" Ogier alisema.

Ogier aliibuka wa kwanza kwene mashindano ambayo yalitamatika mnamo Juni 27 mjini Naivasha.

Hafla hiyo ya siku tatu ilishuhudiwa na maelfu ya Wakenya ambao walijitokeza kushabikia mashindano hayo ya kwanza baada ya miaka 19.

Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria hafla ya kutunza washindi na akaahidi kuwa mashindano ya magari ya kidunia yatakuwa yanafanyika kila mwaka.