logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wamiliki wa Newcastle United wasihi mashabiki wasivae mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu wakati wa mechi

Mavazi kama hayo yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo21 October 2021 - 08:37

Muhtasari


  • •Mavazi kama hayo yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

Newcastle United imewaomba mashabiki wasivae "mavazi ya kitamaduni ya Kiarabu au vazi la kufunika kichwa linalotumika Mashariki ya Kati" kwenye mechi kufuatia kununuliwa kwa kilabu hiyo na wamiliki kutoka Saudi Arabia.

Wafuasi wengine wa Magpies walivaa nguo hizo wakati walipokusanyika nje ya St James Park 'kusherehekea kununuliwa kwa kilabu hiyo

Mavazi kama hayo pia yalionekana wakati wa mechi dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kwanza wa kilabu chini ya wamiliki wapya.

"Hakuna mtu katika kikundi kipya cha wamiliki aliyekerwa kwa njia yoyote," kilabu ilisema.

"Ilikuwa ishara ambayo ilikubaliwa kuwa nzuri na ya kukaribisha kwa nia yake.

"Walakini, kuna uwezekano wa kuwa kuvaa hivi sio sawa na kitamaduni na kuna hatari ya kukasirisha wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved