Cristiano Ronaldo: Sishindani na Messi

Muhtasari
  • Mwandalizi wa tuzo ya Ballon d'Or pascal Ferre alitoa madai hayo kwa gazeti la New York Times
Image: BBC

Cristiano Ronaldo ameshutumu muhariri mmoja wa soka nchini Ufaransa kwa kudanganya baada ya kusema kwamba lengo la raia huyo wa Ureno ni kustaafu akiwa na mataji mengi ya Ballon d'Or zaidi ya Lionel Messi.

Mwandalizi wa tuzo ya Ballon d'Or pascal Ferre alitoa madai hayo kwa gazeti la New York Times.

Mshambuliajo wa PSG Lionel Messi alishinda tuzo yake ya saba ya taji hilo siku ya Jumatatu huku mshindi mara tano wa taji hilo Ronaldo akimaliza katika nafasi ya sita.

Mimi hushinda taji la Ballon d'Or kwanza kibinafsi na pili kwa klabu ninayowakilisha, alisema mshambuliaji wa Manchester United Ronaldo.

''Napigania kushinda taji hilo kwangu mimi binfasi na kwa wale wanaonipenda, sipiganii kushinda dhidi ya mtu mwengine''

''Siku ya Ijumaa, Ferre aliambia New York Times : Ronaldo ana lengo moja tu, na hilo ni kustaafu na mataji zaidi ya Ballon d'Or zaidi ya Messi - na najua hilo kwasababu ameniambia''.

Ronaldo alijibu katika mtandao wa kijamii akisema : Pascal Ferre alidanganya , alitumia jina langu kujikuza na kukuza gazeti anallolifanyia kazi.

''Haikubaliki kwamba mtu anayehusika kutoa tuzo muhimu kama hiyo anaweza kudanganya kwa njia kama hiyo, hakika ni kumkosea heshima mtu ambaye ameheshimu soka ya Ufaransa na tuzo ya Ballon d'Or''.

"Lengo langu kuu ni kushinda mataji ya kitaifa na kimataifa ya klabu ninazoziwakilisha na kwa timu yangu ya taifa.

''Lengo langu kuu ni kuwacha jina litakaloandikwa katuka historia ya soka''.

The Ballon d'Or - ni tuzo inayopatiwa mchezaji bora wa soka wa mwaka - hupigiwa kura na waandishi 180 kote duniani na hutolewa na shirika la soka nchini Ufaransa .

Messi alikuwa ameshinda taji hilo zaidi ya mchezahi mwengine yeyote na tuzo yake ya saba baada ya kuibuka mshindi 2009, 2010, 2011, 2012, 2015 and 2019.

Ronaldo, ambaye mara ya mwisho alishinda tuzo hiyo 2017, alimaliza nje ya wachezaji watano bora duniani kwa mara ya kwanza tangu 2010.