logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Welbeck amtakia heri njema Mwepu baada ya kulazimika kustaafu soka kutokana na ugonjwa wa moyo

Nahuzunika sana kwa sababu ya Enock, Mchezaji mzuri na mtu mzuri sana - Welbeck.

image
na Davis Ojiambo

Michezo12 October 2022 - 09:02

Muhtasari


  • • Familia na afya ni muhimu zaidi kuliko mpira wa miguu - Welbeck alisema.

Wikendi iliyopota Sanaa ya spoti ulimwenguni ilisikitishwa na habari za kuvunja moyo kutoka nchini Uingereza amabpo kiungo wa kati katika klabu ya Brighton & Hoven, Enock Mwepu alitangaza kustaafu kusakata soka mapema kutokana na tatizo la ugonjwa wa moyo.

Mwepu ambaye ni rais wa Zambia aliweka wazi kwamba tatizo la ugonjwa wa moyo ni la kurithi katika familia yake na kuwa madaktari wake walimsihi kuikatisha safari yake katika malimwengu ya usakataji kabumbu kwa sababu ya afya yake.

Dunia ilisikitishwa sana na taarifa hizo ambazo kwa kweli hazifurahishi ikizingatiwa kwamba kiungo huyo alikuwa bado na umri mbichi wa miaka 25 tu!

Wadau katika soka kote ulimwenguni wameungana naye na kumtakia shufaa ya haraka na wengine wakimtakia mema katika maisha yake mengine kando na spoti, huku jumbe zao zikiwa zi za kutia huruma na kuchochea hisia.

Mchezaji mwenzake katika klabu hiyo, mshambuliaji Danny Welbeck aliachia ujumbe kupitia kurasa zake mitandaoni akionesha kusikitishwa kwake na taarifa hizo huku akisema Mwepu alikuwa kama familia kwao.

Welbeck alisema kwamba kufuatia ushauri wa madaktari, wachezaji wenzake hawakuwa na lingine bali kumtakia kila la kheri Mwepu katika maisha mapya ila akasikitika kwamba itawachukua muda kukubali kuwa mchezaji huyo alilazimika kustaafu mapema.

“Nahuzunika sana kwa sababu ya Enock, Mchezaji mzuri na mtu mzuri sana. Familia na afya ni muhimu zaidi kuliko mpira wa miguu. Enock atang'ara nje ya uwanja pia. Hakuna shaka!” Welbeck aliandika kwenye Facebook.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved