logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ngumi ya 'Sugunyo' yampa gari Bondia Karim Mandonga

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuzawadiwa huko kwa Mandonga.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo18 January 2023 - 03:48

Muhtasari


  • • Mandonga sasa anamiliki gari kwa mara ya kwanza alilozawadiwa leo na mmoja wa wadau wa ngumi Tanzania.
  • •Ushindi dhidi ya Mkenya Wanyonyi ni mechi ya kwanza kwa bondia huyo kucheza nje ya Tanzania.

Bondia Karim Mandonga wa Tanzania sasa anamiliki gari kwa mara ya kwanza alilozawadiwa leo na mmoja wa wadau wa ngumi Tanzania.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuzawadiwa huko kwa Mandonga.

Bondia huyo mwenye maneno na tambo za mbwembwe amerejea nchini Tanzania baada ya kutoka Kenya alikokwenda kupigana kwa mara ya kwanza kwenye pambano lake lisilo la ubingwa dhidi ya Daniel Wanyonyi. Alishinda kwa TKO kwa ushindi uliompa heshima.

'Namshukuru Mungu nilicheza kama niko Tanzania, nilitangaza ngumi yangu ya kigeni ikitoka Ukraine inaitwa Sugunyo, nashukuru mwenyezi mungu kwa hatua aliyonipa', alisema Mandonga baada ya kukabidhiwa gari hiyo.

Ushindi dhidi ya Mkenya Wanyonyi ni mechi ya kwanza kwa bondia huyo kucheza nje ya Tanzania, alikofanikiwa kujaza ukumbi mkubwa wa KICC Nairobi. Inakadiriwa zaidi ya watu 2,500 walijitokeza kushuhudia pambano hilo la Mandonga na Wanyonyi.

'Ni mechi yangu ya kwanza kucheza, ya kuonyesha maajabu ya kuimbiwa nyimbo ya taifa, machozi yalinitoka, ni tukio kubwa', alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved