Kufuatia makosa kadhaa ya VAR wikendi iliyopita katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza, EPL, mkuu wa marefa Howard Webb alitangaza mkutano wa lazima na marefa wote na tayari mageuzi kadhaa yameshafanyika.
Jarida la Daily Mail sasa linaripoti kuwa refa mmoja aliyekuwa anahusika na VAR katika mechi za wikendi kwa jina John Brooks amevuliwa mamlaka yake kuelekea mechi kuu ya Jumanne kati ya Arsenal na Manchester City.
Refa huyo wa VAR alitarajiwa kuongoza maamuzi ya VAR katika mechi ya usiku wa jana baina ya Everton na Liverpool na pia kuongoza mechi ya leo baina ya Arsenal na City lakini amevuliwa majukumu hayo huku Webb akiendelea kufanya mageuzi ya kudhibiti makosa Zaidi ya uamuzi wa VAR.
Andre Marriner na David Coote walichukua majukumu ya VAR badala yake kwa Liverpool v Everton usiku wa jana na pia kwa mchezo wa Arsenal dhidi ya Man City Jumatano jioni, mtawalia.
Chama cha marefa kwenye ligi ya premia PGMOL kilithibitisha habari hiyo katika taarifa, ikisema: “John Brooks ameondolewa kwa VAR katika mechi zote mbili za Liverpool v Everton usiku wa leo na Arsenal v Manchester City Jumatano jioni. Andre Marriner na David Coote watachukua majukumu ya VAR badala yake usiku wa leo na Jumatano mtawalia. Kutokana na ratiba ya Jumatatu jioni, miadi ya mechi za wikendi itatangazwa kesho,” Mail walinukuu taarifa hiyo.
Joto lilipozidishwa kwenye VAR wikendi hii, Chelsea pia walikuwa wahasiriwa wa mabishano baada ya Tomas Soucek kuonekana kuumiliki mpira eneo la hatari wakati wa sare ya 1-1 Jumamosi.