Winga wa kimataifa wa Algeria na timu ya Manchester City Riyad Mahrez alifadhiliwa nauli ya treni na mama yake mwaka 2009 wakati anakwenda majaribio ya kujiunga timu ya kwanza ya soka huko Ufaransa.
Kipindi hicho, mchezaji huyo alikuwa chipukizi na hakuwa na lolote mbele nyuma na alihitaji msaada wa mama yake kufanikisha safari yake kwenda kufanyiwa majaribio ili kuanza rasmi safari yake ya soka kama mchezaji wa kulipwa.
Kulingana na wavuti wa Africa Facts Zone, mchezaji huyo alisema mama yake alimlipia nauli ya Euro 160 ambacho kwa sasa ni kiwango sawa na shilingi elfu 24 pesa za Kenya, ili kusafiri kwa treni kuwahi katika timu ambayo ilikuwa inashiriki kwenye divisheni ya nne nchini Ufaransa.
Mahrez anadaiwa kumwambia mamake kwamba endapo angefanikiwa katika majaribio hayo na kupata mkataba, basi angemrudishia mama yake hizo hela za nauli.
Alisema "Nilimwambia mama yangu, usijali, nitakulipa. Nitafanikiwa. Leo nimemlipa" Mahrez alikumbuka akimwambia mama yake maneno hayo baada ya kuwahi mkataba mnono kwenye timu ya Manchester City mwaka 2018.
Mahrez ambaye moja ya wachezaji wanaotegemewa sana kwenye timu ya taifa ya Algeria na pia kwenye klabu yake ya ManCity alichipukia kama kiungo muhimu katika kampeni ya Leicester City kuelekea ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza mwaka 2016 na miaka miwili baadae akajiunga na Manchester City ambapo ameshinda mataji ya ligi ya Premia kwa mara kadhaa.
Gumzo hili la mchezaji kumkopa mama pesa linakuja kipindi ambapo mchezaji wa Morocco Achraf Hakimi amekinukisha kwa kumwandikia mama yake urithi wake badala ya mke wangu.